About Me

Friday 4 September 2015

FRIDAY, SEPTEMBER 4, 2015

Jinsi ya kukabili hisia za umbo dogo la uume


By Dk Shita Samwel
Leo nitafunga mfululizo wa mada juu ya udogo wa maumbile kwa kueleza mambo machache ya kufanya kukabiliana na hali hiyo.
Kama nilivyoeleza hapo awali, kuwa hakuna njia au dawa za uhakika zenye ufanisi kwa ajili ya kuongeza urefu na upana wa uume, inayokubalika na vyombo vikubwa vya afya duniani mfano Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Lakini vipo vitu vichache vinavyoweza kufanyika kwa yule anayedhani au aliyethibitika kuwa ana tatizo hilo, angalau kumpunguzia kadhia hiyo.
Jambo la msingi ni kuongea na mwenza wako ambaye kwa pamoja mna malengo ya kuishi pamoja. Mueleze kwa lengo la kujiweka wazi kwake. Hii ni njia ya kujiweka huru zaidi. Kuficha jambo, inakufanya kuwa na hofu na kukosa kujiamini. Hali hiyo inaweza kushusha msisimko wako wa tendo lenyewe pamoja na matatizo mengine, ikiwamo kufika mshindo mapema na kukosa hamu.
Epuka kuonyesha au kujadili tatizo lako la maumbile kwa wenzako wanaoweza kukukejeli na kukunyong’onyeza kutokana na kujihisi au kuwa na maumbile madogo. Mara nyingi wenye matatizo haya wanakuwa na unene uliopitiliza na uwapo wa kiriba tumbo na kusababisha mwili kumeza shina la uume na kuonekana mfupi.
Kupunguza mwili kwa mazoezi na mlo ni jambo muhimu, kunakufanya kupata mwili imara usio na unene na kukuongezea kujiamini. Kuepuka unene kunaondoa ile hali ya uume kumezwa na mwili.
Ikumbukwe pia mazoezi hayakufanyi tu uonekane mkakamavu bali pia hukuongezea uwezo wa kulifanya tendo kwa ufanisi.
Uwapo wa msitu wa nywele sehemu za siri inaweza kukufanya uonekane na umbile dogo la uume hivyo kuipa picha macho yako kuwa una uume mdogo, wakati si hivyo.
Ni vyema kuweka mazingira hayo kwa kufyeka msitu huo ili uweze kuonekana vyema. Kufanya hivi pia kunasaidia kuongeza msisimko wa maeneo hayo na kukuweka msafi wa kimwili.
Ongea na wataalamu mbalimbali kwani kudhani kuwa una uume mdogo ni kawaida kukosa furaha na kukusababishia matatizo ya kisaikolojia. Zungumza na mshauri mwenye taaluma, mwanasaikolojia, daktari wa magonjwa ya akili na watu wazima waliokuzidi kiumri. Wataalamu hawa watakapokushauri na kukuthibitishia kuwa huna tatizo lolote, hii itakusaidia kuwa na uhakika kuwa, huna uume mdogo kama akili yako inavyofikiria.
Wataalamu waliobobea kwa masuala ya mahusiano huweza kukushauri mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na tatizo lako na wakati huohuo pia wakikusaidia kuepukana na udanganyifu wa mitaani juu ya dawa zinazorefusha na kuongeza unene wa uume. Ni vizuri kuongozana na mwenza wako katika huduma za afya kwani wataalamu hawa ndio watakaokuelimisha na kukupa mbinu za kuweza kukabiliana na hali hiyo.
Wanaume wengi wana imani kuwa kuongeza maumbile kutawafanya waonekane ndio marijali au kuwavutia wanawake. Lakini nafasi ya kuwamo katika wastani wa uume wa kawaida ni mkubwa kwa wanaume wengi wanaodhani kuwa wana uume mdogo. Hata kama ikitokea uume wako ni mdogo kuliko wastani wa kawaida, hiyo haijalishi kwa mwenza wako, kwani unaweza kumridhisha kwa mbinu nyingi. Uthibitisho wa kitaalamu unaonyesha kuwa wanawake wengi sehemu yenye msisimko wa kipekee ipo ndani kidogo tu kati ya inchi 2 hadi 3 kutokea nje ya uke. Kwa sababu hiyo haihitaji uume kuingia umbali mrefu.
Kwa wale wenye uume mrefu huingia ndani hadi kugusa mlango wa uzazi. Eneo hilo halina msisimko wowote zaidi ya kumsababishia mwanamke maumivu.

No comments:

Post a Comment