About Me

Friday 4 September 2015

FRIDAY, SEPTEMBER 4, 2015

‘Afrika Mashariki unganeni kupambana na ujangili’

Tembo katika moja ya mbuga zilizopo Afrika ya
Tembo katika moja ya mbuga zilizopo Afrika ya Mashariki. Tembo ni miongoni mwa aina ya wanyama wanaoathirka sana na shughuli za kijanagili. 
By Mussa Juma
Arusha. Nchi za Afrika zimetakiwa kubadilishana uzoefu wa kudhibiti vitendo vya ujangili wa tembo na faru la sivyo, wanyama hao watapotea Afrika.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Adelhelm Meru alitoa wito huo jana alipokuwa akifungua warsha ya kupitia mpango kazi wa kudhibiti ujangili katika nchi za Afrika iliyopewa jina la Cobra III.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Allan Kijazi alisema ni wajibu wa wadau kudhibiti hali hiyo.
Alisema Taifa pekee haliwezi kudhibiti ujangili na usafirishaji wanyama kwani biashara hiyo, inafanywa kwa ushirikiano wa majangili wa mataifa mbalimbali.
Awali, mkurugenzi kikosi kazi cha makubaliano ya Lusaka ya kukabiliana na ujangili, Bonaventure Ebayi alisema watuhumiwa zaidi ya 300 wa ujangili wamekamatwa.
Alisema kwa sasa baadhi ya nchi za Afrika, Bara ya Asia, Ulaya na Marekani zimeongeza ushiriki katika vita dhidi ya ujangili na kuzuia biashara haramu ya wanyama.
Juni mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alizindua kampeni mpya ya kupambana na ujangili ili kuongeza ufahamu na kuelimisha jamii kuhusu tatizo hilo.
Kampeni hiyo iliwashirikisha wasanii, viongozi wa dini na wadau wa maliasili ndani na nje ya nchi, mwakilishi kutoka China na Balozi wa Marekani nchini.
Wasanii walioshiriki katika kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘Ujangili unatuumiza sote’ ni mwanamuziki Ali Kiba, Vanessa Mdee na Jackline Mengi.
Pia wananchi walitakiwa kutoa ushirikiano ili kuleta matokeo chanya katika kampeni hiyo.

No comments:

Post a Comment