About Me

Tuesday 3 November 2015

UMASIKINI




Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya Binaadamu kama vile chakula,mavazi,huduma za afya,maji safi na makazi.
Umaskini unajihusisha hasa na sababu zinazojihusisha kiwango cha chini cha Uzalishaji kwa watu maskini.
Ni kweli uongozi mbaya na watu wa tabaka la juu ni kikwazo kikubwa kwa watu na familia maskini.
Kundi hili huwa halina sauti na wanakosa kujaliwa na wenye vipato vya juu.Ninahe mama Salma katika kijiji cha mbozi mkoani mbeyambae yeye amekumbwa na tatizo la umasikini ana haya ya kusema                                        Lakini vilevile kutokuwepo kwa Uhuru wa Kiuchumi ni tatizo kwa wajasiriamali miongoni mwa watu maskini.
Ni huohuo umaskini unaosababisha afya duni,ukosefu wa elimu pamoja na ukosefu wa chakula. Hivi vyote ni vitu muhimu kuvipata,kwa mfano tatizo la ukosefu wa elimu limekuwa ni moja ya ongezeko la matumizi ya madawa ya kulevya.
Vijana wake kwa waume hujiingiza katika vikundi viovu vya uvutaji Sigara,Bangi,Kokeni na kujidunga Sindano.
Haya yote hutokea pale vijana kuwa hawana shughuli za kufanya ambazo zitawaingizia kipato katika maisha yao.
Uchunguzi umedhihirisha ya kuwa watoto watoto wanaotoka katika familia au jamii maskini wanakabiliwa na tishio kubwa la kutofanya vyema katika masomo yao.




No comments:

Post a Comment