About Me

Tuesday 3 November 2015

TATIZO WA ELIMU TANZANIA


Mfumo wa elimu bado ni tatizo ,mfumo huu uliopo haumfanyi au kumfundisha mwanafunzi kuweza kufanya kazi bila ya kuajiriwa.
Mfumo bora wa elimu ni ule unaowapa wanafunzi mbinu za kufanya kazi hata kama wamekosa ajira wawe wabunifu kutafuta ufumbuzi wa kujiajiri wenyewe.
Mbali na hayo maisha ya shuleni kumekuwa na changamoto nyingi kama ukosefu wa waalimu wa kutosha.
Waalimu wengi wamekuwa wakijibebesha masomo ambayo hawana uwezo nayo pamoja na kufundisha masomo yasiyopungua matatu.
Hali hii inawafanya wanafunzi kushindwa kuelewa na kufahamu yale masomo ambayo hayana waalimu wenye sifa.
Kutokana na hali hiyo pia inaonyesha kwamba waalimu wengi licha ya kuwa na changamoto zinazowakabili wao wenyewe ila hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na masomo yanayofundishwa kwa lugha ya kiingereza.
Kwa hivyo hilo pia ni miongoni mwa matatizo ya kufeli kwa wanafunzi.
Lakini mbali na hayo kumekua na tatizo la Ufisadi wa kuhujumu kiwango cha elimu nchini.
Hujuma hizi ziko katika Wizara nzima ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo huleta ubaguzi wa kitabaka na kidini.
Ubaguzi huu hutumiwa katika chombo cha Baraza la Mitihani La Taifa.
Chombo hichi hutumia nafasi yake kinyume na sheria na taratibu za umma.
Wanafunzi wengi hupunguziwa viwango vya ufaulu na kufelishwa kwasababu ya ubaguzi wa kitabaka,kijinsia na kidini.
Utabaka huo umeaza tangu kabla ya Uhuru na bado mpaka sasa upo katika sekta zote.
Kabla ya Uhuru elimu ilitolewa kwa kuzingatia matabaka hasa tabaka la rangi na wenye fedha ambapo mwaafrika(mtu maskini) alikuwa daraja la mwisho kupata elimu.
Takwimu kutoka Wizara ya Elimu inaonyesha kuwa Wazungu(matajiri) hawakusomesha watoto wao hapa nchini bali walipelekwa nje.
Hili limebainishwa na hata Waaziri wa Elimu wa sasa Mh.Shukuru Kawambwa wakati akitoa taarifa ya sekta ya Elimu nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar Es Salaam.
Kwa hivyo tunagundua yakuwa hizi ni njama za viongozi wetu na watu wenye fedha kuwadumaza kielimu wananchi kwani maafa na athari za kukosa elimu kwa watoto wao zinaepukika kwasababu watoto wao wanasomeshwa nje ya nchi,na inaonyesha ndiyo hizohizo pesa zetu za kodi wanazosomeshea watoto wao nje ya nchi.
Ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne umekuwa mbovu na wakutisha katika miaka 2010-2012.
Mwaka 2010 Wanafunzi 354042 waliofanya mtihani wa Taifa kidato cha nne,wanafunzi 117,021 walipata daraja sifuri sawa na asilimia 50% ya watahiniwa wote.
Wanafunzi 136,633 ambao ni asilimia 38.6% walipata daraja la nne na kufanya asilimia 88.6% ya watahiniwa wote kupata daraja la nne na sifuri.
Ni wanafunzi 15335 sawa na asilimia 4.3% ndio waliopata daraja la kwanza,pili na tatu.

No comments:

Post a Comment